Mwenyekiti Kamati ya Usajili, Nyika awatoa hofu mashabiki ‘Tshishimbi, Yondani na Kessi ni mali ya Yanga’

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo baada ya wachezaji wao wenye majina makubwa kutarajiwa kuhamia kwenye klabu nyingine wakati huu wa dirisha la usajili wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Nyika amesema kuwa licha ya kushika nafasi ya tatu wapo katika mikakati ya kuhakikisha wanaboresha kikosi chao kwaajili ya msimu ujao huku akiwataka mashabiki kutokuwa na wasiwasi kwa wachezaji, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Hassan Kessi na Tshishimbi kwakuwa bado ni mali ya Yanga.

Tumeshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara  msimu huu kwahiyo tumeangalia makosa yetu na kwa sasa tupo kwenye mikakati ya kutengeneza kikosi chetu kiwe bora zaidi kwaajili ya mwakani.

Mchezaji unapokuwa mzuri kila timu inamuwinda lakini niwatoe wasiwasi wana Yanga kwamba Papy Tshishimbi Kabamba bado anamkataba wa mwaka mmoja Yanga. Juma kashamaliza lakini anaipa nafasi kubwa timu yake kwenye usajili akiwemo Kelvin Yondani kwahiyo wana Yanga wasiwe na wasiwasi iwe kwa Juma Abdul, Yondani, Hassan Kessi na Tshishimbi bado ni mali ya Yanga.

Chirwa mkataba wake umemalizika lakini ametupa nafasi kubwa sisi ya kuongea nae kwaajili ya usajili na kama tukishindwa basi atakwenda sehemu nyingine.

Yanga ambayo inayoonekana kukumbwa na ukata wa fedha msimu huu ina haha kuhakikisha inafanikiwa kuboresha kikosi chake kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi na msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya mwaka huu kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL.

Comments