Wambura njia panda kupata rufaa ya maadili

Image result for wambura photos
Aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ambaye amefungiwa maisha kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu, bado yupo njia panda kutokana na maamuzi ya rufaa yake kwenye kamati ya maadili ya rufaa kutotangazwa hadi sasa.

Wambura amesema baada ya kamati ya rufaa ya maadili kusikiliza shauri lake alitegeme maamuzi ya kamati hiyo yangetangazwa baada ya sikukuu za Pasaka.

“Tulipomaliza utetezi wetu siku ya Jumamosi (Machi 31, 2018) kama saa 12:30 jioni walituambia tunaweza kuondoka watatoa majibu tusisubiri, ilikuwa Jumamosi halafu  Jumapili na Jumatatu ilikuwa ni sikukuu kwahiyo Jumanne wangeweza kutoa majibu, sasa bado hawajatoa tusubiri kidogo wanaweza wakatoa”-Michael Wambura.

“Sisi tulitoa utetezi wetu vizuri kwa kufuata vifungu vya sheria upande wa TFF nao walijaribu kujibu hoja zetu, kilichobaki ni kamati kuangalia hoja zetu kitu ambacho naimani kwamba kamati haitakuwa wao ndio wanajibu hoja. Wajibu hoja walipaswa kuwa ni TFF kwa hiyo kamati haitawajibia hoja TFF.”

“Si dhani kama wataruhusu mambo ambayo hayakuzungumzwa pale, kwa hiyo mambo yaliyozungumzwa pale ndio yatakuwa msingi mzima wa hukumu ndio sheria inavyotaka.”

Wambura amezungumzia pia hofu yake juu ya maneno yanayondelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba ameshindwa rufaa yake pamoja na kuchelewa kutangazwa kwa maamuzi.

“Maneno mengi yanazungumzwa mtaani wakati mwingine huwezi kuyapuuza sana kwa sababu waswahili wanasema lisemwalo lipo kama halipo laja. Mimi nasubiri taarifa rasmi.”

Comments