Trump aiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris

power station chimney (file photo)
Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya hali ya tabia nchi.
Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.
Kujitoa katika mkataba huo ilikua ni mojawapo ya ajenda wakati wa kampeni za Trump
 Kujitoa katika mkataba huo ilikua ni mojawapo ya ajenda wakati wa kampeni za Trump
Bw Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti yaliyoimarishwa.
Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira.
Amezitaja China na India.
Waandamanaji walikusanyika nje ya ikulu ya White House  Waandamanaji walikusanyika nje ya ikulu ya White House                

Comments