Picha: Kinachoendelea kwenye msiba wa mzee Ndesamburo

Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo baada ya kufariki dunia jana ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.Watu wamejitokeza nyumbani kwa marehemu huyo.

Nyumbani kwa Marehemu Mzee Philemoni Ndesamburo aliyefariki dunia jana katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi
Picha na Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini:

waombolezaji wakiwemo ndugu wakijiandaa kwenda kutizama mwili wa Mzee Ndesamburo katika HospItali ya Rufaa ya KCMC

Baadhi ya waombolezaji wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakia nyumbani kwa Mzee Ndesamburo

Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini ,Godbless Lema pamoja na mkewe Neema Lema wakiwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini mara baada ya kukutana nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo

Mtoto wa marehemu Ndesamburo ,Ndohorio Ndesamburo akiwaeleza jambo waombolezaji waliofika nyumbani kutoa pole kwa familia

Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Kaskazini,Aman Golugwa akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo

Baadhi ya viongozi wa Chadema wakiwa katika kikao kifupi nyumbani kwa mareheu Ndesamburo

Familia ya marehemu Ndesamburo wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya kutizama mwili wa mpendwa wao

Mkurugenzi wa kampuni ya World Frontier,John Hudson akimfariji ,mtoto wa marehemu Ndesamburo,Lucy Owenya nyumbani kwao eneo la Mbokomu mjini Moshi

Comments