Kesi ya Wema yapigwa kalenda Kisutu

Malkia wa filamu nchini Wema Sepetu Alhamisi hii amepanda tena katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya tatu kusikiliza kesi yake inayomkabili ya tuhuma za kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya.

Mrembo huyo alisindikizwa na baadhi ya waigizaji wenzake akiwemo Neema Ndepanya. Hata hivyo madam Sepenga amekana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa mpaka Julai 14 ndio itasikilizwa tena.
Wema alitiwa mbaroni na jeshi la polisi mapema mwezi February mwaka huu na kusota rumande kwa siku saba huku akituhumiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake baada ya kufanyiwa msako mkali.

Comments