Watu 60 wauwawa kusini mwa Libya

Wapiganaji nchini Libya
Wapiganaji nchini Libya
Habari kutoka Libya, zinasema kwamba yamkini watu 60 wameuwawa, katika mapigano makali kati ya makundi mawili hasimu, Kusini mwa nchi hiyo.
Msemaji wa kundi la Libyan National Army, amesema kuwa uwanja wake wa ndege wa Brak al-Shati, ulivamiwa.
Kundi moja linalojiita Third Force, linasemekana ndilo lililotekeleza shambulio hilo.
Eneo hilo limekuwa likiangaziwa pakubwa kutokana na taharuki inayotanda kati ya wanaounga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa mataifa iliyoko katika mji mkuu Tripoli, na wapinzani wao.
Mapema mwezi huu, kamanda mkuu wa Libyan National Army, Khalifa Haftar, alikutana na kiongozi mkuu wa serikali iliyoko Tripoli, Bwana Fayez al-Sarraj, ili kujaribu kuzima uhasama unaotokota Kusini mwa nchi hiyo.
Ramani ya Libya
Ramani ya Libya
Libya iliingia vitani baada ya kuangushwa kwa utawala wa hayati Kanali Muammar Gaddaffi mnamo Oktoba 20 mwaka 2011.

Comments