Uchunguzi ufanyike vifo vya wanafunzi 32 – Nikki wa Pili

Wakati uzuni ukiwa umetanda kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea mkoni Arusha na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 pamoja na dereva mmoja, Nikki wa Pili ametoa ushauri kwa mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi kubaini chanzo kilicho sababisha ajali hiyo kutokea.

Rapa huyo ambaye pia anatoka mkoani Arusha, amezitaka mamlaka kuchunguza maadili ya aliyekuwa dereva wa gari hilo pamoja na hali ya gari kabla ya kupata ajali.
“Lakini baada ya mazishi lazima uchunguzi ufanyike, kujuwa hali ya gari lenyewe ilikuwaje, maadili ya dereva, na hali ya usimamizi/ukaguzi wenyewe ulikuwaje na hii ichukuliwe kuweka udhibiti kwa watu wote walio chukuwa dhamana ya kulea watoto kwa maana ya shule. Uthibiti na usimamizi, haswa katika mazingira haya ya biashara,” Nikki wa Pili aliandika Instagram.
Mpaka sasa jeshi la polisi halijaeleza chanzo cha ajali hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko mjini Arusha muda huu ambapo anaongoza wananchi wa mkoa huo pamoja na mikoa ya jirani katika kuuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vincent iliyopo mkoani humo.

Comments