SAMATTA: NI MWENDO WA MAGOLI TUU

Image result for MBWANA SAMATTA IMAGE


Mtanzania Mbwana Samatta usiku wa May 7 2017 ameingia uwanjani katika kikosi cha kwanza cha timu yake ya KRC Genk kucheza dhidi ya AS Eupen katika muendelezo wa michezo ya play off ya Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017.

Image result for MBWANA SAMATTA IMAGE

Samatta akiwa na KRC Genk katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya KRC Genk yakifungwa na Jere Uronen dakika ya 18 na mtanzania Mbwana Samatta aliyetumia vyema pasi ya nahodha wake Thomas Buffel dakika ya 58.
AS Eupen walipata goli la kufutia machozi dakika ya 76 kupitia kwa mnigeri Henry Onyekuru, ushindi huo umeifanya KRC Genk kuendelea kuongoza Kundi B kwa kuwa na jumla ya point 19 ilizokusanya kwa kushinda michezo yake sita na kutoka sare mchezo mmoja.

Comments