Rubani aliyeiba ndege ya Usovieti na kuipeleka Japan

Ndege ya XB-70 bomber ina uwezo wa kasi mara tatu kuliko sauti
Ndege ya XB-70 bomber ina uwezo wa kasi mara tatu kuliko sauti
               
Tarehe 6 mwezi Septemba mwaka 1976 ndege ilionekana ghafla kutoka kwenye mawingu karibu na mji wa Hakodate katika kisiwa kilicho kaskazini cha Hokkaido nchini Japan
Ilikuwa ndege yenye injini mbili lakini haikuwa ndege ya kawaida ambayo watu wa Hakodate walikuwa wamezoea kuiona.
Ndege hiyo kubwa iliyokuwa na alama za Muungano wa Usovieti haikuwa imeikana eneo hilo.
Ilitua katika uwanja wa Hakodate. Barabara ya uwanja wa ndege ilikuwa fupi hali iliyolazimu ndege hiyo kuchimbua ardhi ilipomaliza kukimbia kwenye barabara na kusimama mwisho kabisa mwa uwanja wa ndege.


Rubani akachomoza kutoka chumba cha rubani na kufyatua risasi mara mbili hewani kutoka kwa bastola yake.
Dakika kidogo baadaye maafisa wa uwanja wa ndege wakamkaribia. Huu ndio wakati rubami mwenye umri wa miaka 29 Luteni Viktor Ivanovich Belenko wa jeshi la wanahewa wa Usovieti alitangaza kuwa alitaka kuhama.
Ndege hiyo aina ya Mikoyan-Gurevich MiG-25 ndiyo ndege yenye usiri zaid kuwai kuundwa na muungano wa usoviet.

Marekani ilidhani kuwa ndege hiyo ilikuwa na uwezo mkubwaMarekani ilidhani kuwa ndege hiyo ilikuwa na uwezo mkubwa                
Nchi za magharibi ziligundua kitu ambacho kilionekana kama ndege ya MiG-25 miaka ya sabini. Satelaiti za ujasusi zilikuwa zikichunguza viwanja vya usovieti zilichukua picha za ndege zilizokwa zikifanyiwa majaribio ya kisiri.
Zilionekana kama ndege kubwa za kivita na wanajeshi wa nchi za magharibi walikuwa na wasi wasi baada ya kuona kitu fulani: mbawa kubwa.

Comments