Raia wa Marekani akamatwa Korea Kaskazini

Kim Hak-song ndiye raia wa nne wa Marekani mpaka sasa kukamatwa nchini Korea Kaskazini kwa makosa mabali mbali.

Kim Hak-song akiwa chini ya ulinzi wa Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imesema kuwa imemkamata raia wa hao kutokea Marekani kwa kushukiwa kufanya vitendo viovu dhidi ya taifa hilo. Kim Hak-song, ambaye ni raia wa Marekani, alikuwa akifanya kazi katika chuo cha sayansi na Teknolojia cha Pyongyang PUST na alikamatwa siku ya Jumamosi
Raia wengine watatu wa Marekani kwa sasa wanazuiliwa nchini Korea Kaskazini akiwemo Kim Sang-duck, ambaye alikuwa mhadhiri katika chuo cha PUST. Kukamatwa kwa Kim kunakuja huku kukishuhudiwa msukosuko kati ya Korea Kaskazini na Marekani.
Korea Kaskazini imeitisha kufanya majaribio ya kombora la nuklia huku Marekani nayo ikituma meli ya kivita eneo hilo kuizuia Korea Kaskazini kuunda zana za nuklia.

Comments