Msichana wa miaka 10 anayetaka kutoa mimba India

Maandamano dhidi ya ubakaji wa watoto
Jopo la madaktari linakutana India kuamua iwapo mtoto wa miaka 10 aliyebakwa na babake wa kambo anaweza kuruhusiwa kutoa mimba.
Msichana huyo alibakwa mara kadhaa na babake wa kambo na anatarajiwa kujifungua katika kipindi cha miezi minne ijayo
Sheria ya India haikubali utoaji mimba baada ya wiki 20, ila tu ikiwa maisha ya mwanamke mja mzito yamo hataraini.
Sheria hii kali ilipitishwa ili kuwezesha usawa wa jinsia zote, kiume na kike.
Kumekuwa na mila na desturi India ambapo wanawake wengi wamekua wakitoa mimba punde wanapogundua wanabeba mimba ya mtoto msichana.
Katika miezi ya karibuni, Mahakama ya Juu ilipokea maombi ya wanawake kadhaa waliodai kupata mimba baada ya kubakwa.
Wanawake hao walitaka kutoa mimba zilizopita wiki 20.
 
Mahakama imekua ikituma maombi haya kwa jopo la wataalamu wa afya.
Kesi ya sasa kutoka jimbo la Haryana, madaktari wanakutana kuamua ombi la familia ambayo inataka mtoto wao wa miaka kumi kutoa mimba.
Habari za mimba hii zilitolewa na mamake msichana huyo ambaYe alimpeleka mwanawe hospitalini baada ya kulalamika maumivu ya mwili.
Duru zinasema msichana huyo amekua akiishi nyumbani wakati mamake akiwa kazini ambapo ni kijakazi.
 
Alimuambia Mamake kwamba babake wa kambo amekua akimbaka kila mara na kumtisha asiseme lolote.
Mwanamume huyo amekamatwa na anazuiliwa korokoroni baada ya mkewe kumshtaki kwa unyanyasaji huo anaufanya.

Comments