Maseneta wataka Michael Flynn ahojiwe

Marekani
Michael Flynn
                
Maseneta wanaochunguza uhusiano uliopo kati ya Rais Donald Trump na Urusi wamemwagiza aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama nchini Michael Flynn afike mbele yao kuhojiwa.
Wanataka atoe stakabadhi alizo nazo.
Bwana Flynn alikataa kufanya hivyo majuma mawili yaliyopita.
Alilazimishwa kujiuzulu mnamo Februari baada ya kusema uongo juu ya mawasiliano yake ya simu na balozi wa Urusi nchini humo.
Wakati huo huo;
Aliyekuwa mkuu wa idara ya upelelezi nchini Marekani, James Comey, aliyetimuliwa kazini Jumanne, amejibu hatua hiyo kwa kuwaandikia barua maafisa katika idara hiyo na rafiki zake.
Alisema hatapoteza wakati wake juu ya hatua iliyochukuliwa au jinsi ilivyotekelezwa na akasema kuwa kwa muda mrefu ameamini kuwa Rais ana kila sababu ya kumtimua kazini mkurugenzi wa FBI kwa sababau moja au hata bila sababu yo yote.

Comments