MABAKI YA MFALME MWAMBUSTA WA BURUNDI KUSALIA SWITZELAND

Mfalme Mwambutsa IV wa Burundi
Mfalme Mwambutsa IV wa Burundi

Mahakama moja nchini Switzerland imekamilisha mzozo wa kisheria kuhusu hatma ya mwili wa mfalme wa Burundi aliyeondolewa madarakani, Mwambitsa IV aliyefariki miaka 40 iliopita kwamba atasalia nchini humo kulingana na shirika la habari la AFP ambalo limenukuu chombo kimoja cha habari nchini humo.
Mfalme Mwambutsa aliongoza Burundi hadi uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1962, lakini akaondolewa mamlakani miaka minne baadaye kufuatia mzozo uliodaiwa kutoka kwa uhasimu uliopo kati ya Watutsi na Wahutu.
Alifariki nchini Switzerland 1977, huku akiwacha wasia kwamba mwili wake usipelekwe nchini Burundi.
Mwanawe wa kike na serikali ya Burundi wametaka mabaki yake kurudishwa hadi nchini Burundi akidaiwa kutaka kuchukua mazishi yake kuandaa sherehe ya kuleta maridhiano ya kitaifa.
Mpwa wa mfalme huyo amepinga mpango huo akisisitiza kuwa matakwa ya mfalme huyo lazima yaheshimiwe.
Huku kukiwa na mzozo huo uliosababisha kufukuliwa kwa mwili wake 2012, mabaki ya Mwambutsa yamehifadhiwa katika chumba kimoja cha kuhifadhia maiti mjini Geneva kwa kipindi cha miaka 5 kulingana na AFP.

Comments