Leo ni miaka 36 tangu kifo cha Bob Marley, tujikumbushe haya

Siku ya leo, ni miaka 36 tangu kufariki dunia kwa Mfalme wa muziki wa Reggae, Bob Marley toka nchini Jamaica.
Bob Marley
Historia fupi
Robert Nesta “Bob” Marley alizaliwa February 6 mwaka 1945 na mama mweusi aliyeitwa Cedella Booker na baba wa Kizungu aliyeitwa Norvall Marley. Wakati akiwa mdogo, marafiki zake walimpa jina la utani kama ‘Tuff Gong’.
Alianza muziki miaka ya 1960 akiwa na kundi lake la kina Wailing Wailers, ambalo alilianzisha akiwa na marafiki wawili, Peter Tosh na Bunny Wailer. Mwaka wa 1962, Bob Marley na kina Wailing Wailers wakafanikiwa kurekodi nyimbo zao mbili za kwanza zilizoitwa “Judge Not” na “One Cup of Coffee”.
Bob alimuoa Bi. Rita Anderson mwaka 1966 na akajiunga na kundi akiwa kama mwitikiaji. Kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto watano. Mmoja kati ya hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji wa reggae maarufu.
Mwaka wa 1974, pamoja na kundi la Wailers kutengana, Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers na kujiunga upya na wanachama wapya huku wakindelea kupiga muziki kama kawaida. Mwaka wa 1975, Bob Marley akatoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimpa umaarufu duniani kote, ulijulikana kama “No Woman No Cry”.
Baadhi ya nyimbo zake kali ni pamoja na “I Shot the Sheriff”, “Could You Be Loved”, “Stir It Up”, “Jamming”, “Redemption Song”, “One Love” na, “Three Little Birds”.
Bob Marley alifariki katika hospitali ya Cedars of Lebanon Hospital huko mjini Miami, Florida, kwa tatizo la melanoma (kansa ya ngozi)Hapa Chini tumekuwekea video zake nane, kazi ni kwako.

Comments