Kwa nini Trump ana msimamo mkali dhidi ya Iran?

Rais Donald Trump amekuwa akiikosoa Iran tangu alipochaguliwa kuiongoza Marekani
Hii ni ziara ya kwanza ya rais Donald Trump katika eneo la mashariki ya kati na haitakuwa ya mwisho.
Lakini tayari ameweka wazi kitu kimoja.
Chuki dhidi ya Iran ni kitu kimoja ambacho washirika wa Marekani wanakubaliana.
Kuishutumu Tehran imekuwa swala muhimu akiwa Saudia na Israel.
Uadui dhidi ya Iran ndio gundi inayoshikanisha ule muungano kati ya Israel, Saudia na mataifa madogo ya ghuba.


Lakini haijulikani ni muda gani, mshikamano huo utachukua kudhibiti siasa za eneo hilo.
Swala la pamoja la kuidhibiti Iran ni kitu kimoja lakini je, muungano huo utafanikiwa katika kuleta mwamko mpya katika eneo zima la mashariki ya kati?
Kwa bwana Trump kuikosoa Iran kunamaanisha maswala tofauti.
Kwanza kunamfanya kuonekana shupavu duniani.
Shupavu zaidi ya mtangulizi wake Barrack Obama anayeamini alitia saini mkataba mbaya zaidi katika historia, ule wa kinyuklia na Iran.
Rais Hassan Rouhani amechaguliwa kuiongoza Iran kwa muhula wa Pili Rais Hassan Rouhani amechaguliwa kuiongoza Iran kwa muhula wa Pili                
Pia kunamfanya kuyahakikishia mataifa ya Arabuni na Israel kwa mara moja kuhusu maslahi yao.
Pia kunatoa hakikisho jipya kuhusu harakati za kuafikia amani kati ya Israel na Palestina mbali na kutuma onyo kwa Tehran kuhusu sera zake katika eneo hilo ambazo Marekani inadai zinakiuka maslahi yake.
Hatahivyo ukweli ni kwamba rais Trump sasa ameanza kugundua ukweli uliopo.
Ijapokuwa sera ya kigeni ya bwana Trump bado inaendelea.
Ziara hii ya sasa katika eneo la mashariki ya kati bado inafuata utaratibu kwa kuwa ni mapema mno kwa yeye kujiingiza katika siasa za eneo hilo.
Hivyobasi mbali na mikataba ya mabailioni ya fedha inayotiwa saini ni funzo gani haswa tunalopata?
Licha ya matamshi yote aliyotoa, ukweli ni kwamba sera ya kigeni ya rais Trump inatekelezwa kwa tahadhari kubwa.

Kwa mfano dalili zote zinaonyesha kuwa mpango wa ubalozi wa Marekani kuhamishwa hadi katika eneo la Jerusalem umesitishwa kwa muda.
Vilevile, inakuwaje Marekani inaliuzia taifa la Saudia silaha wakati ambapo linapigana huko Yemen?
Matumaini ya mamlaka ya rais Trump ya kuweka amani mashariki ya kati yanakinzana na wataalam wengi ambao wanajua siasa za eneo hilo vyema.
Wanadai kwamba Israel na Palestina haziko tayari kuafikiana ili kuweza kufikia amani ya kudumu.
Wengine wanasema kuwa badala ya kulipa kipau mbele swala la amani ambalo itabidi kutoa majibu ya maswala nyeti kama vile Jerusalem na wakimbizi, lengo hilo halifai kuwa na matumaini makubwa kama vile kuanza na mpango wa muda ambao utasababisha kuwepo kwa maafikiano ya amani ya muda mrefu.
Lakini haijulikani iwapo utawala mpya wa Marekani una subira ya kutosha ya kuwepo kwa majadiliano hayo.
Hivyobasi swala hilo linaturudisha tena kwa Iran. Je utawala wa Trump una sera gani dhidi ya Iran?
Licha ya marais wote kushutumu mpango wa Iran wa nyuklia, Je Trump ana uwezo wa kuukimbia?
Saudia inafurahishwa na msimamo mkali wa Marekani dhidi ya IranSaudia inafurahishwa na msimamo mkali wa Marekani dhidi ya Iran                
Ukweli ni kwamba uchaguzi wa rais wa Iran Hassan Rouhani atakayehudumu kwa muhula wa pili huenda ukazidi kufanya mambo kuwa magumu.
Hatahivyo alionekana kuwa mgombea wa pekee mwenye msimamo wa kadri katika uchaguzi huo hata iwapo kiongozi wa dini wa taifa hilo anashikilia maamuzi makubwa kuhusu sera ya kigeni.
Rais Rouhani tayari ameanza kuwarai wanasiasa wa mataifa ya Ulaya kuanzisha mazungumzo kuhusu kuifungulia vikwazo vyote Iran.
Hatua hiyo huenda isikubalike na Marekani.

Lakini kuna swala tata katika eneo hilo ambalo rais Trump hushindwa kuliangazia.
Serikali ya Iraq ni mshirika mkuu wa Marekani dhidi ya wapiganaji wa Islamic State.
Lakini Iran pia nayo inaunga mkono Iraq na imetuma majeshi yake na washauri kusaidia katika vita vyake.

Comments