Aliyekuwa rais wa Korea Kusini afikishwa mahakamani kuanza kesi

Park Geun-hye arrives in court in Seoul (23 May 2017)
Bi Park alifikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu
Rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.
Hii ndio mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu kuondolewa madarakani na kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu. Amekanusha kufanya makosa yeyote.
 
Bi Park alifika mahakamani akiandamana na rafiki wake wa karibu, Choi Soon-Sil ambae anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni makubwa.
Park Geun-hye (left) and Choi Soon-sil (right) in court in Seoul (23 May 2017)Bi Park Geun-hye (kushoto)na Choi Soon-sil (kuliat) wakiwa mahakamani                
Alipofika mahakamani Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hana hajaajiriwa.
Yeye na rafiki wake huyo hawakuzungumziana na walikaa kando ya mawakili wao. Rais huyo wa zamani alivalia mavazi meusi na siyo sare za wafungwa ambazo amekua akivalia gerezani.
 
Alikua pia na kibandiko cha nambari yake ya mfungwa 503. Nywele zake zilifungwa kwa kipini kilichotolewa na mamlaka za gereza. Kwa sasa kiongozi huyo anakumbwa na njiya panda baada ya kuondolewa kwenye ikulu.
Choi Soon-sil on trial in Seoul (18 April 2017)
Choi Soon-sil alifikishwa mahakamani mapema mwaka huu

Comments