TIMU NNE ZILIZOFANIKIWA KUINGIA FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE



Usiku wa April 19 2017 michezo ya pili ya robo fainali ya UEFA Champions League ilichezwa barani Ulaya, FC Barcelona waliwakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia wakati AS Monaco walikuwa wenyeji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani katika michezo hiyo ya marudiano.
Barcelona ambao walikuwa wanahitaji ushindi wa kuanzia goli 4-0 ili wasonge mbele dhidi ya Juventus kutokana na mchezo wa kwanza kufungwa kwa magoli 3-0, wamejikuta wakiaga mashindano kwa kulazimishwa sare tasa ya 0-0, huku Dortmund wao wakiomdolewa katika hatua hii kwa ggregate ya 6-3.
Dortmund wao mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani walipoteza kwa kukubali kufungwa magoli 3-2, hivyo mchezo wa marudiano walipaswa kupata ushindi walau wa magoli 2-0 ili wasonge mbele, bahati haikuwa kwao na wamejikuta wakiambulia kipigo cha magoli 3-1, ratiba ya nani atacheza na nani itajulikana ijumaa hii.

Comments