OPCW: GESI YA SARIN ILITUMIKA ILITUMIKA KWENYE MASHAMBULIZI YA SYRIA

Walioathirika wengi wao ni Watoto
Walioathirika wengi wao ni Watoto

Majibu ya uchunguzi nchini Syria yanaonyesha kuwa Gesi ya Sarin au kemikali ya kufanana na hiyo ilitumika kwenye silaha za kemikali kutekeleza mashambulizi nchini Syria mapema mwezi huu, Shirika la kuzuia matumizi ya silaha za kemikali (OPCW) limeeleza.
Sampuli kutoka kwa waathirika 10 zimefanyiwa tathimini katika maabara nne, mkuu wa Shirika hilo Ahmet Uzumcu ameeleza.
Shambulio katika mji unaodhibitiwa na waasi, Khan Sheikhoun liligharimu maisha ya watu takribani 87.
Majeshi ya Syria yalikana kutumia gesi ya kemikali.
Mshirika wa Syria, Urusi imesema shambulio la anga lilipiga ghala lenye silaha za kemikali la waasi , lakini utetezi huo ulikataliwa.
Picha za Video zilionyesha raia wengi wao watoto wakikohoa na kutokwa povu mdomoni
Shirika la OPCW linaendelea kufanya mahojiano na kukusanya sampuli

Comments