HAJI MANARA ATOA SALAAM KWA WADAU

hajismanaraHaji Manara

Salaam wadau,

kesho jnne usiku pale Amaan Stadium patachezwa mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi baina ya klabu kongwe zaid kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki, Simba na Yanga.
Ni mechi ya tano kwa miamba hiyo ya soka kukutana kwenye uwanja huo wenye historia pana sio Zanzibar tu, bali hata Tanzania kwa ujumla.
Mara ya kwanza klabu hizi zilikutana mwaka 1975 kwenye fainali ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, ambapo Yanga ilishinda kwa goli mbili kwa bila, magoli yakifungwa na marehemu Gibson Sembuli na baba yangu Al Haji Sunday Ramadhan Manara Computer, ni mechi iliokuwa kali na nilijuzwa ndio asili ya kumeguka kwa Simba na kuundwa klabu ya Nyota Nyekundu.
Zama hizo babu yangu mzaa mama marhumu Hassan Haji alikuwa mwenyekiti wa Simba, na wanachama wa Simba wakahoji ktk mkutano mkuu kwa nn Sunday atufunge kila siku au kwa kuwa ni mkwe wa Mwenyekiti? Taarifa ya maneno hayo yaliibua sintofahamu kubwa klabuni, hali iliopelekea wanachama waasisi wa klabu(waswahili kwenda kuanzisha klabu yao ya Red Star. Ikumbukwe game ya Zbar ilichezwa muda mfupi baada ya fainali ya ligi ya taifa pale Nyamagana Stadium Mwanza, ambapo Yanga ilifungwa na Simba 2-1, kwa magoli ya Sunday na Sembuli,
Moja ya jambo lingine la kukumbukwa kwenye mchezo huu ni kuzaliwa kwa mwandishi wa makala hii siku Yanga ikicheza na Mufurila Wonderess kwenye nusu fainali ya kombe hilo, ambalo Simba ndio timu ya kwanza kulitwaa na Bingwa wa kihistoria wa muda wote wa ukanda huu murua. Mechi ya pili miamba hii kukutana ilikuwa pia ktk fainali ya kombe hili, na Simba kulipa kisasi kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya Penati 6-5, huku mkwaju wa mwisho ukikoswa na beki wa Yanga, David Mwakalebela, Mungu alinijaalia kuishuhudia mechi hii kabambe mno pale Zbar, nikishuhudia ufundi wa hali ya juu katikati ya uwanja,baina ya Hussen Masha, Michael Paul, Ramadhani Lenny kwa upande wa Simba, na Issa Athman, Method Mogella, Steven Mussa na Hamis Gaga kwa upande wa Yanga, kwangu hii ilikuwa mechi bora kuwahi kuishuhudia baina ya watani hao, ikumbukwe dakika 120 zilishuhudia sare ya 1-1, huku Simba ikitangulia kwa goli la Hussen Masha na Yanga wakisawazisha kwa goli la Said M

Comments