WAGANDA WATUMIA KINGA HII BADALA YA KONDOMU

Matumizi ya condom imekuwa ikishauriwa sana kwa muda mrefu kama njia ya kusaidia mtu kujikinga na maradhi ya kuambukiza kati ya watu walio kwenye uhusiano.
Kutoka Kiyindi, Kampala Uganda stori ambayo iko tofauti kidogo ni hii ishu ya watu kubuni kitu tofauti, badala ya condom wao wanatumia condom bandia, wamezibuni wenyewe kutokana na mifuko ya plastiki wanaziita ‘buveera’.

Mahitaji ya condom ni makubwa lakini wenyeji wa eneo hilo wamesema hali ngumu ya kimaisha imefanya washindwe kumudu gharama za kununua kinga hizo.

Ripoti ya Tume ya kuthibiti Ukimwi ya mwaka 2013 ilionesha Uganda inahitaji condom milioni 20 kila mwezi, hata hivyo zinazopatikana hazitoshi, kingine ni kwamba condom zinauzwa bei ambayo kwa watu wenye kipato kidogo hawawezi kumudu.

1729541
Mfanyakazi mmoja wa kituo cha Afya cha jamii amesema kiwango cha maambukizi UKIMWI na kuenea magonjwa mengine ya zinaa katika Wilaya hiyo yako juu sana ambapo ishu ya wahisani kupunguza usambazaji baada ya mtafaruku uliotokana na Serikali kuzuia uhusiano wa jinsia moja.
wpid-couples-love-21461550-500-375

Comments