Siku Ya UKIMWI Duniani,Tanzania ‘Tamaduni Na Mila’ Zinachangia Ongezeko La Maambukizi

world-aids-day
Ikiwa leo ni siku ya UKIMWI, Duniani ambapo Tanzania Kitaifa siku  hiyo inafanyika Mkoani Njombe Juhudi  za kupambana na maambukizi ya ukimwi mkoani humo  zimezidi kushika kasi kutoka katika mashirika mbalimbali na kuanza kuungana na viongozi wa mila ili kutokomeza mila hatarishi.

Akizungumza na East Africa Radio katika viwanja vya Sabasaba mkoani njombe,  afisa uhusiano wa PSI kanda ya nyanda za juu kusini, Sanday Beebwa amesema kuwa katika vitu vinavyo ongeza kasi ya maambukizi mkoani humio na Tanzania kwa ujumla ni pamoja na tamaduni na mila.

Maadhimisho haya ambayo kilele chake ni leo  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais  Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

Comments