QUEEN DARLEEN AELEZA SABABU YA KUKATAA ZAWADI HIII....

queen darleen 
Siku ya leo msanii Queen Darleen anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, tumebahatika kufanya nae mahojiano na tumemuuliza ni vitu gani hua anafanya siku kama ya leo na Queen alisema ” Siku kama ya leo inapofika saa 6 (Usiku) kama mwili wangu haupo msafi basi natia udhu  kisha naanza sala na kumuomba mwenyezi Mungu kwa sababu kuna kuugua na pia kuna kufakwa najaribu kumuomba mwenyezi Mungu anisaidie uhai mrefu”

Alipoulizwa kuhusu kama atafanya sherehe, Queen Darleen alisema ” Sijawahi kufanya sherehe mimi kama mimi lakini leo marafiki zangu wakina Mwasiti, Almasi, K Star Diamond kina shilole wote wameamua kunifanyia kitu hapa nyumbani kwangu kuanzia saa 2 usiku, mi sijui ni kitu gani watanifanyia. Kwa hiyo suprise lakini nimesema sitaki zawadi ya gari, nimeshampa warning kabisa Diamond”


Comments