PENNY:DIAMOND HANA CHAKE HAPA


Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.
MTANGAZAJI aliyewahi kujiachia kimalovee na Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amesema mwanamuzi huyo kwa sasa alie tu kwani ameshachumbiwa na hawezi kumpata tena.Kauli ya mwanadada huyo ilikuja baada ya kuulizwa kama
anaafikiana na kauli ya mama wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu kwamba, kwa kuwa Wema kamuacha Diomond basi staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo bora akampose yeye.

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Mmh! Hapa suala la Diamond kurudiana na mimi halipo kabisa maana simhitaji yeye wala mwanaume mwingine yeyote, mimi ninaye wangu tayari ambaye ameshanichumbia hivyo sitarajii kabisa kuwa na mwingine zaidi yake,” alisema Penny.

Comments