JACKLINE WOLPER APEWA ZA MBAVU..SHUKA CHINI

image
Kwako mtoto mzuri unayekimbiza kwenye anga la filamu Bongo, Jacqueline Massawe Wolper.
Bila shaka ni mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.

Binafsi mimi naendelea vizuri mambo yanakwenda kwenye mstari na leo nimekukumbuka kupitia barua nzito . Nataka kusema na wewe mawili matatu
ambayo mimi nimeona si sawa kufanywa na wewe!
Nisichelewe sana wala nini, madhumuni ya
barua hii kwanza kabisa ni kutaka
kukukumbusha kwamba unapaswa
kujiheshimu katika kila sekta kwa kuwa
wewe ni kioo cha jamii .
Jamii inakuheshimu , inakufuatilia kila
hatua unayopiga maishani .
Wanaokufuatilia ujue wanakupenda ingawa
pia hata wale wasiokupenda nao pia wanakufuatilia.
Wanakufuatilia kwenye vyombo vya habari ,
katika mitandao ya kijamii na hata live
mitaani. Kauli yako lazima iwe na staha. Sababu ya kukwambia jiheshimu ni kauli
zako kwenye mitandao ya kijamii . Mara kadhaa nimekuwa nikiona ukiposti lugha ya
matusi kwa waliokuudhi . Kwa nini utukane ?
Kwa mtu anayejiheshimu kama wewe si busara hata kidogo kutukana hata kama umechokozwa.Akili yako inapaswa kutafakari kwa kina
kabla ya kuposti kitu chochote katika mitandao ya kijamii .
Unapoposti kitu pia
ujue kuna watu ambao watakipenda na
ambao hawatakipenda, sasa kwanza
kuwajibu wale wasiokipenda unajishushia
heshima!
Mfano mzuri ni siku ile ulipoweka aina mpya ya simu katika mtandao wa kijamii .
Niliufuatilia mjadala ule, kuna watu walikuponda kwamba aina ya simu hiyo
mpya haipo na kwamba ulifanya hivyo ili kujipa sifa.
Mtoto wa kike ukaona bora umtukane,
ukaandika tusi zito kabisa kumjibu shabiki
huyo. Ukimjibu mjinga unategemea nini ?
Najua kabisa dhamira yako kuweka simu
hiyo ilikuwa ni utani lakini walivyoipokea
baadhi ya mashabiki wakakusababisha
utukane.
Wewe unaheshimika , kutukana si jambo la
busara. Siku hizi teknolojia inakua, ni rahisi mtu kukufuatilia na kukupata na
hata kukuchukulia hatua za kisheria. Kwa nini utukane? Kwanza hata ukiamua
kutukana, utatukana wangapi katika mitandao ya kijamii ? Si sawa !
Siku hizi mitandao inatumika kama chombo cha biashara , ni vyema ukawa
makini na unavyoposti ili ikiwezekana hata
ukatumia mitandao hiyo kujiingizia mkwanja kuliko kutukana na watu
wanaokuheshimu wakakuona hauna maana .
Usipoteze muda wako kuwajibu watu ambao hawakosi cha kuongea . Utajisumbua
tu, fuata mifano ya mastaa wengi
ulimwenguni, wanapoweka kitu katika mitandao ya kijamii huwa hawageuki kutazama watu wamekomenti nini baadaye.
Weka kitu chako kisha fumba macho kama huoni vile, si wote watakaokichukulia kitu
chako chanya. Kuna wengine wataponda au watakutukana, ukiwajibu watu watakuona
wewe mpuuzi kuliko hao waliokuanza !
Kwa leo acha niishie hapo , kuwa makini sana na mitandao ya kijamii .

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI

Comments