CHEKI PICHA MPENZI ANYONGA DEMU WAKE NA KUMTUPA HUKO KIGOMA

 
Baba mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuua mpenzi wake kwa kumnyonga na kumtumpa katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.

Taarifa za awali zinasema kulikuwa na ugomvi baina yao hao wapenzi wawili hali iliyopelekea mwanamke (Mama Koku) kumshtaki mwanaume mahakamani na kusababisha Mwanaume kufungwa miezi miwili jela. Siku kadhaaa baada ya mwanaume kutoka gerezani alipata habari kuwa mpenzi wake huyo aliyesababisha kuwekwa ndani anatembea na mwanaume mwingine ndipo mwanaume huyo alipopanga njama/namna ya kutekeleza mauwaji hayo.

Taarifa zinasema mara baada ya mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililo kinyume na neno la MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20.13 alimwambia mpenzi wake kuwa; "Leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari"  Mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza maisha.

Comments