WANYAMA ATOLEWA UWANJANI NA MAPOLISI,HUKU KOCHA WA TIMU HIYO AKITIMULIWA

KIUNGO Victor Wanyama aliokolewa na Polisi baada ya mashabiki wenye hasira wa timu yake ya taifa, Kenya kuvamia Uwanja kufuatia Harambee Stars kutolewa na vibonde Lesotho katika hatua za Awali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mashabiki wa Kenya walivamia Uwanja baada ya dakika ya safe ya 0-0, timu ya Wanyama ikiwa imetoka kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza.
Police waliingia uwanjani na kumuokoa Wanyama anayechezea Southampton ya England na kumsindikiza kutoka uwanjani. Kocha Adel Amrouche, alifukuzwa baada ya mechi.
Lesotho sasa itaungana na Uganda, Botswana, Sierra Leone, Malawi, Msumbiji na Rwanda, kwenda kwenye makundi ya kuwania tiketi ya AFCON mwakani nchini Morocco 




Comments