QUICK ROCKA AANZISHA NGUO ZA KAMPUNI YAKE

1168856_227967090708631_704454781_n
Rapper Quick Rocka amezindua nguo za kampuni yake ‘Switch Clothing Line’ alizozipa jina la ‘Switch Like Me’.
Akiongea na Kikwetu Blog, Quick amesema kwa kuanza ameanza na t-shirt za rangi mbalimbali ambazo tayari zipo sokoni. “Tumeanza na t-shirt lakini ndani ya mwezi nimeplan kufanya kitu kikubwa zaidi. Tunataka kufanya kwa quality kubwa, kwenda kuprintia China ambayo itakuwa ni t-shirt na kofia pia,” amesema Quick.
Pamoja na biashara ya t-shirt, Quick Rocka alifungua studio yake ya muziki iitwayo Switch Studio.

Comments