MGONJWA WA EBOLA ALIYEPONA ATENGWA

 
Wakati virusi vya Ebola vikiendelea kusambaa katika Afrika Magharibi na kusababisha taharuki miongoni mwa wakazi wa nchi zilizokwisha kuathirika na ambazo bado hazijaathirika katika ukanda huo, baadhi ya walioupata gonjwa huo wamepona lakini pamoja na kupona bado hiyo haiwafanyi kukwepa kunyanyapaliwa.

Mmoja ya wanafunzi wa udaktari ambaye amepona ugonjwa wa Ebola na kupewa cheti cha kuruhusiwa na kituo kilichokuwa kikimpa matibabu huko nchini mwake Guinea lakini amejikuta katika wakati mgumu kurudi katika maisha yake ya kawaida kwa kuwa watu wanamkimbia ikiwemo shule anayosoma wakimwambia abaki nyumbani.
"Tunanyanyapaliwa na unajua wanapotutizama kama hivyo, unajua, hata familia yangu, watu wananitenga. Ninajisikia mpweke, wakati mwingine ninaenda matembezini. Ninaishi na Mjomba, wazazi wangu wanaishi kijijini. Nyumbani niko peke yangu, ninakula peke yangu na ninapohisi mambo hayako sawa ninaenda kutembeatembea. Shuleni wameniambia nikae nyumbani nitibiwe. Niko nyumbani tangu nilipoumwa. Siwezi kupata hata mahali pa kufanyia mazoezi yangu ya masomo kivitendo," Amesema mwanafunzi huyo

Comments