JAMAA AUMBUKA BAADA YA KUMLIPIA DEMU NAULI AKAJUA ATAPATA NAMBA YA SIMU


Tumepanda daladala moja, ikafika wakat wa konda kuchukua mchango wa mafuta....kimbembe kikaanzia hapo, mdafada kajisachi weeeee nauli hana akaanza kumbembeleza konda kuwa atamlipa akifika mwisho wa safari.


Konda akagoma na akaanza kutoa maneno ya dharau kwa yule dada, nikaona hapa ndo nakamatia fursa, nikamlipia yule demu halafu nikamchimba mkwara mzito sana konda huku nikitishia kumtandika na makofi, nikajifanya namfahamu sana yule dada.

Lengo langu ni kwamba tukishuka nachukua contact fasta, maana kwa kweli demu alikuwa ni mkali kinoma, tulipofika mwisho wa safar akaniomba tuongozane, nikajua yees kumbe hata yeye kanimaindi....tukafika kwny duka flani.

Nikasikia analiambia jamaa flan tuliolikuta pale dukani:- baby yani nilitaka kuadhirika....asingekuwa huyu hata cjui ingekuwaje, akalisimulia kila kitu huku kajiegesha kwny kifua cha huyo boya, mi natukutia kwa hasira, alipomaliza kulisimulia likambusu mdomoni.

Halafu eti likanipa mkono kunishukuru, likatoa wallet na kunipa sh elfu tano, ina maana huyo dada alidhani nimemkopesha ile mia nne,au alitaka kunidhalilisha mbele ya yule boya.

Ina maana yeye hawezi kujiongeza kuwa kuna mengineyo nilitaka yaendelee behind the scene, au alijua mi ni mlokole, au alitaka nijue ana mtu wake, mxxxxxxxxxiiiiiiiuuuu, bado nina maswali mengi sana juu ya hilo.
(FROM MDAU

Comments