AUNTY AMPA ONYO MKE WA MOSE IYOBO


Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kuvamiwa na kundi la watu akiwa nyumbani kwa Wema Sepetu akitaka kuadabishwa kwa madai ya kutembea na mume wa mtu, msanii huyo ameamua kumuandikia waraka mwenye mume.

Aunt alifikia uamuzi wa kuandika waraka huo baada ya siku chache baadaye tena kuandikwa habari juu ya kunaswa jijini Mwanza akiwa na mnenguaji wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moze Iyobo ambaye ni mume wa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mwengi.
Waraka huo ambao unapatikana kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu:
“Dah! Kwa nini mimi kila siku, mimi kweli jamani hakuna wengine huko? Basi utashindwa hata kusalimiana na watu ktk hii dunia na yote ni wewe dada wa Mbagala, Mwengi.

Mnenguaji wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moze Iyobo akimchumu mke wake, Mwendi.

Una nini lakini na mimi, unapita unaongea uongo wee nakunyamazia, sio kama ni mpuuzi ila najitahidi kulinda kaheshima kangu hakahaka kalikobaki hebu nenda ‘kadeal’ na wa dizain zako plz mimi sitaki Mwengi, sitaki mm sio mnuka jasho mwenzio. Ni ngumu sana kuyapata unayoyataka. Mume mume, tukilala mume, tukiamka mume, we unamjua mume wewe au! Dah yaani ngoja niache tu mana naona ndio nazidi kuharibu …. still mimi ni Mrs Demonte na itabaki kuwa hivyo forever.
Ukilizungumzia sakata lake na mke wa mtu huyo, Aunt alisema: “Huyu mwanamke kuna kitu anatafuta, anataka kuniharibia heshima yangu lakini hataweza, mimi ni Mrs Demonte tu.

Moze Iyobo (kulia) akipozi na mnenguaji mwenzake kutoka kikundi cha Wasafi Classic. 

“Si anasema mimi namchukulia mume wake, sasa ngoja nitaweka mtego, nitamchukulia kwelikweli ili kama ni kukinukisha akinukishe kihalali.”

Comments